Page Number :3

Dar es Salaam News

Zaira ya Waziri wa Mambo ya nje wa Iran - Tanzania
Zaira ya Waziri wa Mambo ya nje wa Iran - Tanzania
Amir-Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwasili katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam nchini Tanzania akitokea Bamako, mji mkuu wa Mali. Punde baada ya kuwasili Amir-Abdollahian alikaribishwa rasmi na Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kongamano la kumbukizi ya kifo cha Imam Khomeini (RA) lafanyika nchini Tanzania
Kongamano la kumbukizi ya kifo cha Imam Khomeini (RA) lafanyika nchini Tanzania
Kwa mnasaba wa kukumbuka miaka 33 ya kufariki dunia Ayatullah Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kushirikiana na Idara ya Falsafa na Mafunzo ya Dini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Falah
Programu ya Quran Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kadhia ya Qudsi
Programu ya Quran Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kadhia ya Qudsi
Sheikh Abdul Nour Salim, Mmisionari wa Kiislamu alisisitiza umuhimu wa kusoma Qur'ani Tukufu hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati kitabu cha Mwenyezi Mungu kiliteremshwa. Akaongeza kusema: “Kusoma Qur’ani katika miezi mingine kuna manufaa mengi, lakini katika mwezi huu manufaa yake yameongezeka zaidi ya maradufu. Sheikh Abdul Nour amesimulia kisa cha Palestina na kusema: Msikiti wa Al-Aqswa licha ya kuwa kibla cha kwanza cha Waislamu, ni sehemu takatifu ambapo Mtume Mtukufu rehema na amani ziwe juu yake, katika safari yake ya kutoka Msikiti Mtukufu hadi. Msikiti wa Al-Aqsa, uliswali mahali hapa patakatifu pamoja na mitume wengine.
Barua kuhusu Quds
Barua kuhusu Quds
Barua ya Qudsi
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu na kauli mbiu ya mwaka mpya
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu na kauli mbiu ya mwaka mpya
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyid Ali Khamenei, ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1401 Hijria Shamsia na akaupa mwaka huo jina la mwaka wa "Uzalishaji wa Kutegemea Teknolojia na Utengenezaji Ajira".
Mazazi ya Imam Mahdi (AJTFS)
Mazazi ya Imam Mahdi (AJTFS)
Imam Muhammad Mahdi (a.s) alizaliwa siku ya Ijumaa ya mwezi 15 Shaaban mwaka 255 Hijria mjini Samarra Iraq na baba yake akiwa ni Imam Hassan Askari (a.s). Imam Mahdi ni mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupitia kizazi cha masharifu na masayyid cha binti mtukufu wa Bwana Mtume Muhammad y
 Dar es Salaam Maonesho ya Sanaa na Ufundi
Dar es Salaam Maonesho ya Sanaa na Ufundi
Katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Mwanamke Duniani Kituo cha Utamaduni cha Iran Dar es Salaam kwa kushirikiana na Safina Kimbokota & Neviindie Godrich wamefanya Maonesho ya Sanaa ambayo yamefanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Iran kilichopo Upanga Palm Beach, Siku ya Jumanne Tarehe 8 Machi 2022, Tunachukua nafasi hii kuwashukuru sana washiriki wote haswa Ubalozi ya Indonesia, Rais wa Shirikisho la ufundi na Sanaa Tanzania - TAFCA, Dada Safina Kimbokota, Alliance française na Ndiekacha
Mazazi ya Bi Fateh Zahraa (AS)
Mazazi ya Bi Fateh Zahraa (AS)
Kituo cha Utamaduni ch Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kilifanya Sherehe za Mazazi ya Bi Fatima Zahraa (AS) siku ya Jumamosi ya Tarehe 22 Januari 2022 Semina hiyo hiyo ilihudhuriwa na Wanawake mbalimbali wa Dar es Salaam, kutoka madhehebu ya Suni, Shia, Bohra na Wengineo. Semina hiyo yenye kichwa cha habari FAMILIA NA HAKI YA MWANAMKE na wanawake mbalimbali walichangia juu ya mada hiyo. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wanawake mbalimbali akiwe Naibu Waziri Mstaafu mama Shamim Khani, mama Riziki Shahari Waziri Mstaafu, Mama Maryam Alvandi mke wa Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapa Tanzania, Marziye Pirani Mke wa Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran na wengineo.

:

:

:

: