Ziara fupi ya Kituo cha Utamaduni
Mwambata wa Kituo cha Utamaduni cha China leo mapema saa 5 asubuhi amefanya ziara katika Kitu cha Utamaduni cha Iran
- Mgurenzi wa Kituo cha Utamaduni wa Ubalozi wa China nchini TanzaniaWang Siping na ujumbe wake leo hii walikuwa na ziara fupi katika Kituo cha Utamaduni cha Iran hapa Dar es Salaam.
- Alipokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Mkurugenzi Mwambata wa Kituo cha Utamaduni cha Iran hapa Dar es Salaam Bwana Morteza Pirani, Madhumu hasa ya viara hii hii fupi ya Bwana Wang Siping ni kuja kubadilishana uzoefu na Mwambata wa Iran. Ikumbukwe kuwa Iran na China wamekuwa na Uhusiano mzuri na wa muda mrefu sana hasa upande wa Sanaa na utamaduni
- China na Iran ni nchi ambazo zinatamaduni za muda mrefu na Iran imetumia nafasi hii kuwaeleza kuhusu Iran na miji mbalimbali ya Iran
- Katika Kikako cha waambata hawa wawili walimetumia nafasi hii kukuaribisha Bwana Siping kutembelea Iran ambapo alimuonesha baadhi ya Maeneo ya Iran katika vitabu kisha akawamwambia kuwa kutembelea na kujionea mwenyewe kwa uhalisia Iran ilivyokuwa nzuri
- Mwisho Bwana Pirani alimpa zawadi kutoka nchini Iran na Bwana Siping akashukuru kwa mapokezi na ukarimu aliopata katika Kituo cha Utamaduni
Andika maoni yako.