• Oct 13 2023 - 15:45
  • 521
  • Muda wa kusoma : 1 minute(s)

Utawala dhalimu wa Israel unavyo wauwa Wailamu wa Ghaza

Utawala wa kigaidi wa Israel umeua na kujeruhi maelfu ya raia wa kawaida na wasio na hatia wa Palestina na hasa watoto wachanga na wanawake, kwa ajili tu ya kujaribu kufidia na kufunika aibu kubwa

Utawala wa kigaidi wa Israel umeua na kujeruhi maelfu ya raia wa kawaida na wasio na hatia wa Palestina na hasa watoto wachanga na wanawake, kwa ajili tu ya kujaribu kufidia na kufunika aibu kubwa uliyopata kutokana na kufedheheshwa kijeshi na wapiganaji wa Hamas kupitia operesheni yao ya Kimbunga cha al-Aqsa hivi karibuni. Mbali na hayo unatekeleza mzingiro wa kinyama na kijinai dhidi ya Ukanda wa Gaza ambapo umekata maji, umeme na kuzuia chakula kuwafikia zaidi ya wakaazi milioni mbili wa ukanda huo. Jinai zote hizo ambazo bila shaka ni uhalifu wa kivita, zinatekelezwa kinyume kabisa na kanuni na sheria za kimataifa.

Kufuatia mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni, karibu wakaazi elfu tano wa Ghaza wameuawa shahidi au kujeruhiwa, wengi wao wakiwa ni raia wa kawaida hasa watoto na wanawake, na kufikia sasa hakuna sura zozote maalumu za wanachama wa Hamas au makundi mengine ya muqawama zinazoonekana kati ya wahanga hao waliouawa shahidi. Dalili kuu ya hilo ni kuwa wengi wa wapiganaji hao ima wako mstari wa mbele wa vita katika operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa, au wako nyuma ya mstari huo kwa ajili ya kutoa misaada ya dharura na wako tayari kabisa kukabiliana na adui Mzayuni.

 

Ni jukumu la Maimamu wote kuombea amani Palestina na kuzungumza kuhusu hii kadhia ya Ghaza

 

تانزانیا دارالسلام

تانزانیا دارالسلام

Andika maoni yako.

Ingiza maandiko yako Kisha bonyeza Enter

Mabadiliko ya ukubwa wa maandiko:

badilisha nafasi za maneno:

Badilisha urefu wa mistari:

Badilisha aina ya panya: