Barua kuhusu Quds
Barua ya Qudsi
Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa ya kusisitiza juu ya kukombolewa Quds Tukufu, na hilo ndilo lengo kuu la Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran: inawaalika Waislamu na wapenda amani na uhuru kote duniani hususan wananchi wa Iran kushiriki kwenye matembezi ya Siku ya Quds.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
"Ametakasika aliyemchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyouzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona".
Kukombolewa Quds Tukufu kutokana na uchafu wa wavamizi , lilikuwa lengo tukufu, daghadagha na wasiwasi uliopo katika miaka kadhaa iiyopita, ni kuiona Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa mstari wa mbele katika kuwaunga mkono wananchi waliodhulumiwa wa Palestina na harakati hiyo kusambaa ulimwenguni kote. "Kukombolewa Quds" kunaweza kupatikana kwa kutumia njia ya muqawama na mapambano badala ya kupoteza muda kwa kutumia njia ya mazungumzo na maadui wanaoupiga vita Uislamu, Utu na Ubinadamu.
Kukombolewa Quds, sio tu kwamba ni lengo kuu, bali kunahesabiwa kuwa ni moja ya mazungumzo ya kuleta maelewano kati ya wahubiri na walinganiaji wa uhuru na wenye kutafuta haki duniani.
Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu), kwa mtazamo huo na kwa mantiki kubwa kabisa, aliifanya siku ya Quds kuwa ni kitovu cha kushikamana mabilioni ya wanadamu duniani kote. Jambo ambalo limepelekea utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel mara kwa mara kukabiliwa na changamoto kutokana na kufanya vitendo visivyo vya kibinadamu dhidi ya Wapalestina.
Leo hii, Quds Tukufu ndio kiini cha mazungumzo ya muqawama na mapambano katika eneo la mashariki ya Kati na duniani kote. Mbali na nusura ya Mola Mlezi, wanamapambano wa Kipalestina wakiwemo Hamas na Jihad Islami katika makabiliano ya kijeshi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, wanaopata uungaji mkono wa nchi za Kimagharibi na vibaraka wao wa eneo la Mashariki ya Kati , leo hii wamekuwa wakishuhudia mwingiliano wa muqawama ulimwenguni kote. Siku ya Quds ni hatua ya kuangaziwa na kuthibitishwa muungano huu wa pamoja na wenye kuandaa fursa.
Leo, tumeingia katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao sisi ni wageni wa Mwenyezi Mungu, ambapo jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya wakaazi wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan zimeshadidi mno, kambi ya Jenin, eneo la Sheikh Jarrah na hata katika uwanja wa Masjidul Aqswa yamebadilika na kuwa maeneo ya kutekelezwa vitendo vya ukandamizaji dhidi ya wananchi wa Palestina.
Kinyume chake, tunashuhudia kung'aa kwa jina la "Muqawama na mapambano ya pande zote" dhidi ya adui Mzayuni. Mapambano hayo ya pande zote, yanajumuisha vipengee kadhaa: kushuhudiwa satua ya muqawama ndani ya maeneo ya kiistratijia ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu hadi kuonyeshwa kwenye kanali za vyombo vya habari vya wanamapambano juu ya dhulma na ukandamizaji wanaofanyiwa Wapalestina. Mazungumzo ambayo adui hawezi kuyavumilia, ni suala la kukombolewa maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu na kurejea wananchi wa Palestina kwenye ardhi za asili za mababu zao.
Leo hii, kuanzia Harakati ya Hamas ya Palestina na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, hadi kufikia Harakati ya Hashd al Shaabi ya Iraq, Harakati ya Answarullah ya Yemen na wafuasi wa muqawama na mapambano ya Kiislamu duniani kote, wote kwa pamoja wameelekeza nguvu na macho yao huko Quds Tukufu na kwa wananchi wa Palestina. Katika miaka iliyopita na hata hivi karibuni, suala la kufanyika matembezi ya Siku ya Quds,urithi adhimu ulioanzishwa na Mapinduzi ya Kiislamu, umesababisha kuamsha fikra za wanadamu za kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa na kukandamizwa wa Palestina.
Wananchi wa Iran, pamoja na ndugu zao wote katika ulimwengu wa Kiislamu, leo hii watapiga kelele na nara za uungaji mkono wao wa kukombolewa Quds Tukufu na uungaji mkono wa kukombolewa Kibla cha Kwanza cha Waislamu. Kwenye nara hizo, kufanyika mazungumzo eti ya amani kama vile muamala wa karne au mpango wa kuwepo uhusiano wa baadhi ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel, bila shaka mikakati yote hiyo itafeli na haitakuwa na maana yoyote. Hii ndiyo ile ahadi na bishara njema ambayo Mwenyezi Mungu amewapa wenye kutafuta ukweli kwenye Qurani Tukufu, na tutakuwa wenye kulitimiza hilo siku baada ya siku. Inshaallah.
Andika maoni yako.