Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Amirkabir
Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Amirkabir au Tehran Polytechnic ni moja ya vyuo vikuu vya ufundi na teknolojia vya Iran, ambacho kiko katika jiji la Tehran na kilifunguliwa rasmi mnamo 1958. Hivi sasa, takriban wanachuo 14,000 wanasoma katika chuo kikuu hiki katika viwango tofauti vya kielimu.
Vitivo na vitengo vya kielimu
Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Amirkabir kwa sasa kina vitivo 16, idara 6 zinazojitegemea, vitengo 3 vya elimu katika miji ya Bandar Abbas, Garmsar na Mahshahr. Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Amirkabir pia kina kampasi ya kimataifa na kituo cha mafunzo ya elektroniki.
Vituo vya mafunzo vya chuo hicho ni kama ifuatavyo:
• Kampasi ya Usimamizi wa Teknolojia na Uhandisi
o Kitivo cha Uhandisi na Teknolojia
o Kitivo cha Usimamizi wa Elimu na Teknolojia
o Kitivo cha Utafiti na Usimamizi wa Teknolojia na Uhandisi
• Kampasi ya Uhandisi wa Umeme, Kompyuta na Uhandisi wa Zana za Tiba
o Kitivo cha Uhandisi wa Umeme
o Kitivo cha Uhandisi wa Kompyuta
o Kitivo cha Uhandisi wa Zana za Tiba
o Kitengo cha Utafiti ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Mtandao wa Umeme
• Kampasi ya Ufundi wa Mitambo, Anga na Bahari
o Kitivo cha Uhandisi wa Mitambo
o Kitivo cha Uhandisi wa Anga
o Kitivo cha Uhandisi wa Bahari
o Kitengo cha Teknolojia ya Uhandisi wa Mitambo
• Kampasi ya Nyenzo za Kisasa
o Kitivo cha Uhandisi wa Kemia
o Kitivo cha Uhandisi wa Ufumaji
o Kitivo cha Uhandisi wa Rangi
o Kitivo cha Uhandisi wa Nyenzo na Ufuaji wa Metali
o Taasisi ya Utafiti wa Nyenzo za Kisasa
• Kampasi ya Mafuta, Ujenzi na Madini
o Kitivo cha Uhandisi wa Ujenzi na Mazingira
o Kitivo cha Uhandisi wa Madini
o Kitivo cha Uhandisi wa Mafuta
o Taasisi ya Utafiti wa Ujenzi na Ardhi
• Kampasi ya Sayansi
o Kitivo cha Hisabati na Sayansi ya Kompyuta
o Kitivo cha Fizikia na Uhandisi wa Nishati
o Kitivo cha Kemia
o Taasisi ya Utafiti wa Sayansi
• Kampasi Zilizopo Nje ya Chuo Kikuu
o Kampasi ya Mahshahr
o Kampasi ya Bandar Abbas
o Kampasi ya Garmsar
o Kampasi ya Kimataifa
o Kampasi ya Kimataifa ya Kish
Kulingana na matokeo ya hivi karibuni yaliyotayarishwa kwa mfumo wa QS, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Amirkabir kimeshika nafasi ya 477 kati ya Vyuo Vikuu duniani. Aidha Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif cha hapa nchini kimeshika nafasi ya 409 duniani. Hivyo, Chuo Kikuu cha teknolojia cha Amirkabir kinahesabiwa kuwa ni cha pili, kati ya vyuo vya teknolojia hapa nchini. Pia, kulingana na kiwango cha ubora wa vyuo vikuu, uliotangazwa na Taasisi ya Times unaonyesha kuwa, mnamo 2021, Chuo Kikuu cha Amirkabir kiko katika nafasi ya 70 barani Asia na cha nne hapa nchini.
Kiungo cha tovuti ya chuo kikuu:
JIna | Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Amirkabir |
Nchi | Iran |
Uorodheshaji wa Vyuo Vikuu Duniani | 409 |
Aina | Kiserikali |
Jumla ya idadi ya wanafunzi | 14,000 |
Anwani | +98 (21) 64540 |
Tovuti | https://aut.ac.ir/en |
Chagua Kwa Umakini
Upofu wa Nyekndu Upofu wa Kijani Upofu wa bluu Nyekundu Ngumu Kijani Ngumu Kuona Buluu Ngumu Kuona Monochrome Monochrome maalumMabadiliko ya ukubwa wa maandiko:
badilisha nafasi za maneno:
Badilisha urefu wa mistari:
Badilisha aina ya panya: