• Sep 20 2023 - 11:07
  • 346
  • Muda wa kusoma : 1 minute(s)

Mkutano wa UN

Raisi amesema hayo katika hotuba yake mbele ya Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kuongeza kuwa, "Dunia inaelekea katika nidhamu mpya ya kimataifa, na mradi wa kuufanya ulimwengu uwe wa Kimarekani umefeli."

Raisi: Mradi wa kuufanya ulimwengu uwe wa Kimarekani umefeli

Raisi amesema hayo katika hotuba yake mbele ya Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kuongeza kuwa, "Dunia inaelekea katika nidhamu mpya ya kimataifa, na mradi wa kuufanya ulimwengu uwe wa Kimarekani umefeli."

Amesema taifa la Iran kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu linajifakharisha kwa kuwa na nafasi kubwa katika kuwaanika mabeberu Mashariki na Magharibi.

Kadhalika Sayyid Ebrahim Raisi amelaani vitendo vya karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Sweden na Denmark na kusisitiza kuwa, "Tunaamini kuwa, kuheshimiwa matukufu ya kidini kunapasa kuwa moja ya ajenda kuu za Umoja wa Mataifa."

Rais wa Iran amebainisha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inathamini mno usalama wa nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi na kusisitiza kuwa, uwepo wa maajinabi katika eneo si sehemu ya suluhu, bali ni tatizo na uwepo huo unayazidisha mashaka mataifa ya Asia Magharibi.

"Jamhuri ya Kiislamu inakaribisha na kuupokea kwa moyo mkunjufu mkono wa urafiki ikiamini kwa dhati kwamba, uhuru na ujirani mwema unatoa fursa zenye maslahi kwa eneo zima, " ameongeza Sayyid Raisi. 

 

Ameashiria vita vya Ukraine na umuhimu wa kutumia diplomasia kutatua mgogoro huo na kusema: Msimamo wetu ulio wazi kama Jamhuri ya Kiislamu ni kwamba, hatuungi mkono vita vyovyote popote pale duniani ikiwemo Ulaya.

Aidha amelipongeza taifa la Iran kwa kusimama kidete mkabala wa njama za maadui walioibua na kuchochea ghasia mwaka jana hapa nchini, kwa kisingizio cha kifo cha mwanamke wa Kiirani, Mahsa Amini.

Rais wa Iran amesema bayana kuwa: Taifa la Iran liliweza kuzima hujuma kubwa zaidi ya vyombo vya habari na vita vikubwa zaidi vya kisaikolojia katika historia.

 

 

تانزانیا دارالسلام

تانزانیا دارالسلام

Andika maoni yako.

Ingiza maandiko yako Kisha bonyeza Enter

Mabadiliko ya ukubwa wa maandiko:

badilisha nafasi za maneno:

Badilisha urefu wa mistari:

Badilisha aina ya panya: