Chuo Kikuu cha cha Kimataifa cha Imam Khomeini
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Imam Khomeini kilichopo katika mkoa wa Qazvin kilianza shughuli zake za kielimu mwaka 1996 baada ya kupitishwa sheria ya kuanzishwa chuo hicho katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (bunge) la nchi hiyo.Hadi sasa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Imam Khomeini kimeshawapokea wanafunzi wageni kutoka zaidi ya nchi 100 duniani. Wanafunzi kutoka nchi mbalimbali wanasoma zaidi ya fani za kielimu 30 katika kiwango cha shahada ya kwanza, zaidi ya fani 70 katika kiwango cha shahada ya pili (uzamili) na fani 30 za kimasomo katika hatua ya uzamivu na kuna makundi 33 ya elimu katika Chuo Kikuu hicho ambao wanajishughulisha na kujipatia elimu.
Hivi sasa kuna vitivo saba kwenye chuo hicho ambavyo ni Kitivo cha Sayansi na Utafiti wa Kiislamu, Kitivo cha Fasihi na Sayansi ya Binadamu, Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Kitivo cha Sayansi za Msingi, Kitivo cha Ufundi na Uhandisi, Kitivo cha Kilimo na Maliasili, Kitivo cha Usanifu na Mipango Miji na Kituo cha Mafunzo ya Lugha ya Kifarsi kwa wanafunzi wageni. Kuna wanafunzi 6,509 wa Kiirani na 693 kutoka nchi mbalimbali duniani wakisoma katika ngazi za shahada ya kwanza, shahada ya pili na uzamivu, na kuna zaidi ya fani 100 za kimasomo na wanachuo wa kigeni 925 wamepitia katika kozi ya kujifundisha lugha ya Kifarsi kwenye chuo hicho. Vitivo vya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Imam Khomeini vina suhula nzuri na kamili za kujifundishia, zikiwemo zaidi ya maabara 60 zilizokuwa na zana na suhula za kutosha kabisa, bustani za maua na mashamba darasa ya kiutafiti, na zaidi ya vituo 10 vya kompyuta na kumbi za maonyesho. Kuhusiana na kituo cha kujifundisha lugha ya Kifarsi , hadi sasa zaidi ya wanachuo 4,000 kutoka nchi 90 duniani walipokelewa na kupewa mafunzo ya lugha ya kifarsi. Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia imekichagua kituo hicho kuwa ni marejeleo pekee rasmi ya kufundisha lugha ya Kifarsi kwa wageni wanaosoma nchini humo. Hivi sasa, kuna wajumbe 300 wa Bodi ya Wahadhiri wakitoa huduma za kielimu na kiutafiti kwenye chuo hicho, ambapo karibu asilimia 88 ya wahadhiri hao ni maprofesa wasaidizi, aidha wapo wahadhiri waandamizi ambao wamebobea kwenye fani zao maalumu. Licha ya kuwepo wajumbe wa Bodi ya Wahadhiri, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Imam Khomeini kimetunga na kuchqpisha vitabu, makala na kufanya ubunifu mbalimbali wa kielimu katika kiwango cha kitaifa na kimataifa , na kimeshajinyakulia nafasi ya kwanza katika kufasiri vitabu mwaka 2003, na kujipatia tuzo nyingine katika fani za hisabati katika miaka ya 2005 hadi 2010, imechapisha makala 334, chuo hich kimetunga na kutarjumi vitabu 137 na kusajili bunifu 15 kutoka mwaka 2005 hadi sasa. Hayo ni miongoni mwa matunda na mafanikio yaliyopatikana katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Imam Khomeini.
Maktaba Kuu ya chuo kikuu imejengwa katika eneo lenye zaidi ya mita mraba 4060 , na imekusanya aina ya vitabu 115,840 vya Kifarsi na Kiarabu, aina za vitabu 20,398 vilivyoandikwa kwa lugha za kigeni, kuna aina 55 ya magazeti na majarida ya Kifarsi na lugha za kigeni, na zaidi ya majarida na machapisho 8,000 kwa lugha za Kifarsi na kigeni yaliyopo kwenye idara ya masjala. Aidha kuna nyaraka 152 za kiutafiti na tasnifu 3,488 katika nyanja za kielektroniki na hivyo vyote vimehifadhiwa kwenye kanzidata ya chuo hicho.
JIna | Chuo Kikuu cha cha Kimataifa cha Imam Khomeini |
Nchi | Iran |
Aina | Kiserikali |
Jumla ya idadi ya wanafunzi | 7202 |
Idadi ya wanafunzi wa kigeni | 693 |
Anwani | +98 28 3390 1596 |
Tovuti | http://ikiu.ac.ir/tour/ |
Chagua Kwa Umakini
Upofu wa Nyekndu Upofu wa Kijani Upofu wa bluu Nyekundu Ngumu Kijani Ngumu Kuona Buluu Ngumu Kuona Monochrome Monochrome maalumMabadiliko ya ukubwa wa maandiko:
badilisha nafasi za maneno:
Badilisha urefu wa mistari:
Badilisha aina ya panya: