UJUMBE WA MKUU WA TAASISI YA UTAMADUNI NA MAWASILIANO YA KIISLAMU BAADA YA KUUAWA SHAHIDI MWANAHABARI WA KIPALESTINA
Hujjatul Islam Walmuslimiin Muhammad Mehdi Imani Pour Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran ametoa ujumbe kufuatia kuuawa shahidi mwanahabari wa Kituo cha Televisheni cha Al Jazeera huko Palestina. Ujumbe wake ni huu ufuatao:
Hujjatul Islam Walmuslimiin Muhammad Mehdi Imani Pour Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran ametoa ujumbe kufuatia kuuawa shahidi mwanahabari wa Kituo cha Televisheni cha Al Jazeera huko Palestina. Ujumbe wake ni huu ufuatao:
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea”.
Kuuawa shahidi "Shiriin Abu Aqla", mwanahabari mwenye uzoefu mkubwa wa kituo cha Televisheni cha Al-Jazeera, wakati alipokuwa akiripoti jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni huko Jenin, kumefungua pazia jengine la ukatili na dhulma ya utawala huo ghasibu mbele ya macho ya walimwengu.
Kulengwa kwa makusudi Shahidi Shiriin Abu Aqla na Wazayuni kunaonyesha wazi uelimishaji wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na wanafikra katika kuelezea jihadi dhidi ya sura bandia ya utawala unaoikalia Quds kimabavu, umefikia hatua ya utawala huo ghasibu kuingiwa na kiwewe na hofu.
Shahidi Shiriin Abu Aqla anahesabiwa kuwa ni miongoni mwa mashahidi wa Jihad katika kukabiliana na maadui walio dhidi ya utu na ubinadamu, mwandishi wa habari ambaye alikuwa na ustadi mkubwa wa kupigiwa mfano katika kipindi chake chote cha kutekeleza majukumu yake ya kupasha habari za ukandamizwaji wa Palestina na wakaazi wa Quds Tukufu.
Kwa hakika kuuawa shahidi mwanahabari huyu mwanamke kutaacha ujumbe mzito kwenye mabega ya wanajihadi wengine katika uga wa kuelezea jinai za utawala wa Kizayuni, na hatimaye njia hii angavu na takatifu, itakuwa ni kukombolewa Quds Tukufu, na kusafishwa uchafu wa maghasibu wa Kizayuni katika maeneo yote ya Palestina. Inshaallah
Muhammad Mehdi Imani Pour
Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu
Andika maoni yako.