• May 20 2022 - 06:40
  • 372
  • Muda wa kusoma : 5 minute(s)

Mulla Sadra Mwanafalsafa Mashuhuri wa Kiirani

Sadr al-Din Muhammad bin Ibrahim Shirazi, anayejulikana kama “Mulla Sadra”, ni mwanafalsafa, Aaref na mwanzilishi wa shule ya falsafa ya “Hekimat Mutaaliyah”, msomi huyu alizaliwa  miaka kumi na tano ya mwisho ya karne ya kumi Hijria (979 hijria), lakini haijulikani tarehe kamili ya kuzaliwa kwake.

Baba yake Mulla Sadra, Ebrahim Ghavami Shirazi, alikuwa mmoja wa mawaziri wa serikali ya Uajemi akitokea katika familia inayoheshimika ya Ghavami, ambapo pamoja na kuwa na mali, utajiri, heshima, na kuwa mfanyabiashara mashuhuri, hakuwa na watoto kwa wakati huo. Ili kupata mtoto, aliweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu kwamba, iwapo  Mwenyezi Mungu akimjaalia kumpa mtoto mwema  na mwenye maadili mema, atawasaidia maskini na wale wanaotafuta elimu. Mwenyezi Mungu alimjaalia na kumpa mtoto wa kiume ambaye aliitwa Muhammad lakini yeye alimuita "Sadra".

Hali ya kiuchumi na kifedha ya familia ya Mulla Sadra ilikuwa nzuri sana, kwani ni miongoni mwa matajiri wa Shiraz, kwa minajili hiyo aliwatafuta walimu maalumu walikuwa wakienda nyumbani kwao kwa minajili ya kumsomesha Mulla Sadra. Sadru al Din alikuwa kijana mwerevu sana, mwenye hima na juhudi kubwa katika masomo na pia alikuwa mdadisi mno, kwa kipindi  kifupi tu cha masomo yake aliweza kuwa mahiri katika masomo mbalimbali kama vile fasihi ya lugha ya Kifarsi na Kiarabu na sanaa ya kuandika maandishi (kaligrafia).

Mulla Sadra alikuwa bado hajafikisha umri wa balehe alipojifunza kidogo juu ya elimu ya sheria ya Kiislamu (fiqh), mantiki na falsafa na alivutiwa na elimu ya Irfaan ( teosofia). Akiwa kijana mdogo, aliandika maelezo yake ya kumbukumbu ambayo yanaakisi vizuri shauku yake  ya baadaye ya kutaka kujua fasihi ya kiirfani na hasa mashairi ya Kiajemi ya Farid al-Din Attar, Jalal al-Din Moulavi na Iraqi, pamoja na Usufi wa Ibn Arabi.

Mara baada ya kufariki mfalme wa Uajemi, ndugu yake akashikilia wadhifa wa ufalme na akaamua kuelekea Qazvin ambapo wakati ule ulikuwa mji mkuu. Kuna uwezekano mkubwa, baba yake Mulla Sadra alikuwa waziri katika baraza la mfalme huyo. Inaelezwa kuwa, Mulla Sadra alipata elimu yake akiwa kijana mdogo katika mji wa Shiraz na pia katika mji wa Qazvin. Akiwa huko Qazvin, Mulla Sadra alikutana na wasomi na wanazuoni wawili wakubwa ambao ni Sheikh Bahauddin Amili na Mirdamad na akashiriki kwenye darsa zao. Kwa muda mfupi, akawa mwanafunzi hodari aliyewaongoza wanafunzi wenzake kimasomo.

Sheikh Baha'i na Mirdamad walikuwa wajuzi wa elimu zote za zama zao, na kwa kipindi kirefu Mulla Sadra aliweza kustafidi na darsa za Sheikh Mirdamad katika elimu ya falsafa na Irfaan.

Kisha Mulla Sadra,  alielekea  Isfahan pamoja na Sheikh Baha'uddin na Mirdamad kwa lengo la kuongeza elimu yake, wakati huo mji mkuu wa utawala wa Safavi ulipochukua uamuzi wa kuuhamisha kutoka Qazvin na kuupeleka Isfahan. Haijulikani ni miaka mingapi alikaa Isfahan, lakini  kuna uwezekano mkubwa mwaka  wa 1602 Miladia  alirejea kwenye mji wao wa asili wa Shiraz kwa lengo la kusimamia  mali za baba yake. Mulla Sadra aliweza kutoa  sehemu ya utajiri wa mali za baba yake kwa masikini,  ingawa hadi sasa baadhi ya mali zake bado zingalipo huko Shiraz mkoa wa Fars baada ya kuziwekea wakfu.

Mulla Sadra alifundisha kwenye shule yake huko Shiraz, wakati  huo wanafalsafa na wasomi wengi wa kidini  walikuwa wakiiga wanafalsafa wa kabla yake, fikra zake mpya walizikejeli na waliamua kumvunjia heshima kwa sababu waliona ushawishi na nafasi  za wasomi wengine zimo hatarini. Lakini Mulla Sadra hakuwavunjia heshima wapinzani wake, bali alipoona mashinikizo yanaongezeka aliamua kuuhama mji wa Shiraz.

Haijulikani Mulla Sadra alifunga ndoa lini na mwaka gani, lakini kuna uwezekano mkubwa mwanafalsafa huyo alifunga ndoa akiwa na umri wa miaka  arobaini hivi, kwani mtoto wake wa kwanza alizaliwa mwaka 1609 Miladia. Amma baada ya kusumbuliwa na kufanyiwa vitimbi mbalimbali aliamua kuhamia mji wa Qum akiwa na mkewe na mtoto wake. Msomi huyo alichagua kuishi katika kijiji cha Kahak, kilichopo pambizoni mwa mji wa Qum, ambapo Mulla Sadra alibahatika kupata watoto wengine wawili akiwa kijijini hapo. Kwa ujumla Mulla Sadra alikuwa na watoto watano; watoto wa kike walikuwa  watatu na watoto wa kiume walikuwa  wawili. Mirza Ibrahim mmoja kati ya watoto wake, alikuwa msomi mkubwa katika fani za falsafa, fiqh na tafsiri ya Qurani Tukufu katika  zama zake. Mtoto wake mwengine aitwaye Ahmad alikuwa mwanafalsafa, mtaalamu wa fasihi na mshairi, ambapo ameandika vitabu kadhaa vyenye maudhui mbalimbali.

Mji wa Qom katika zama hizo, ulikuwa bado haujakuwa  kituo muhimu cha kielimu na kifalsafa. Hadi sasa mabaki ya nyumba yake ya kifahari aliyoijenga  bado yapo katika kijiji hicho. Huko Qom, alilea wanafunzi wengi, akiwemo Fayyaz Lahiji na Feyz Kashani, ambao wote walikuja kuwa wakwe wa Mulla Sadra.

Kipindi fulani, msomi huyo aliamua  kuacha kufundisha kwa sababu ya kuvunjika moyo kwa masaibu yaliyomkuta na hivyo kuupitisha umri wake wote uliobakia kwa kufanya ibada na kufunga swaumu.

Baada ya kuishi Qum kwa miaka kadhaa, Mulla Sadra aliombwa arudi  kwenye  jamii na huko alianza kuandika, kufundisha, kuchapisha, na kusambaza mafanikio ya  fikra zake.  Baada ya kipindi cha ukimya, aliandika vitabu kadhaa, ikiwa ni pamoja na kitabu chake kikbwa  na “ Dairatul Maarif” ya kifalsafa iitwayo Asfar  na kuandika risala kadhaa zilizokuwa majibu ya wanafalsfa waliokuwa katika zama zake.

Inaonekana kwamba Mulla Sadra alikwenda Shiraz yapata mwaka 1632 Miladia kwa mwaliko wa Allahordikhan  mtawala wa jimbo la Fars, Allahordikhan, kwa shabaha ya  kuendesha shule ya kufundisha falsafa, na huko alianza kufundisha  falsafa, tafsiri ya Qurani Tukufu na  hadithi.

Binti mkubwa wa Mulla Sadra, Umm Kulthum alikuwa msomi, mshairi, na mwanamke mwenye kufanya ibada na zuhudi pia, mumewe alikuwa Mulla AbdulRazaq Lahiji. Binti wa pili wa Mulla sadra, alikuwa anaitwa Zubeda, ambaye mumewe alikuwa  Faydh Kashani (mwanafunzi wa Mulla Sadra) na binti wa tatu aliitwa Maasumeh, alikuwa mashuhuri kwa kuwa na maalumati mbalimbali, mshairi na mwanafasihi.

Mulla Sadra amesafiri  kwa miguu mara saba kuelekea Makka kwa minajili ya kutekeleza Ibada ya Hija katika  kipindi chote cha maisha yake. Katika safari yake ya saba kwenda Makka kutekeleza ibada ya Hija,alipofika katika mji wa Basra (Iraq) aliugua na hatimaye kufariki dunia. Mji  wa Basra wakati huo ulikuwa sehemu ya nchi ya Iran. Imeelezwa kuwa, Mulla Sadra alifariki dunia mwaka 1640 Miladia, ingawa baadhi ya wanahistoria wengine wanasema Mulla Sadra alifariki dunia mwaka 1634 Miladia. Mulla Sadra amezikwa katika mji wa Najaf, kwenye Haram ya Imam Ali bin abi Talib (as).

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeainisha kila ifikapo tarehe 1 Khordad (Kalenda ya Kiirani) Sawa na tarehe 22 Mei, kuwa ni siku ya kumkumbuka mwanafalsafa na msomi huyu mahiri wa Kiirani, Mulla Sa

تانزانیا دارالسلام

تانزانیا دارالسلام

Andika maoni yako.

Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ni moja ya mashirika ya Iran ambayo yanafungamana na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu; na ilianzishwa mwaka 1995. [Ziada]

Ingiza maandiko yako Kisha bonyeza Enter

Mabadiliko ya ukubwa wa maandiko:

badilisha nafasi za maneno:

Badilisha urefu wa mistari:

Badilisha aina ya panya: