• Jun 3 2022 - 16:45
  • 468
  • Muda wa kusoma : 3 minute(s)

KUMBUKUMBU YA KUFARIKI DUNIA IMAM KHOMEINI (MA)

Tarehe 3, Juni 1989, yaani miaka 33 iliyopita, Imam Ruhullah Musawi Khomeini (MA), mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 87. Baada ya kutangazwa habari ya kufariki kwake dunia, ulimwengu wa Kiislamu uligubikwa na wingu la simanzi na huzuni.

Tarehe 3, Juni 1989, yaani miaka 33  iliyopita, Imam Ruhullah Musawi Khomeini (MA), mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 87. Baada ya kutangazwa habari ya kufariki kwake dunia, ulimwengu wa Kiislamu uligubikwa na wingu la simanzi na huzuni. Imam Khomeini alizaliwa tarehe 24 Septemba mwaka 1902 huko katika mji wa Khomein katikati mwa Iran. Alianza harakati zake za kisiasa sambamba na shughuli zake za kielimu na kiutamaduni, katika mji wa Arak na kisha Qum.

Kutokana na shughuli zake za kisiasa zilizokuwa zikiukera sana utawala wa kidhalimu wa mfalme Shah, utawala huo ulimbaidisha Imam katika nchi za Uturuki, Iraq na hatimaye Ufaransa. Katika kipindi cha miaka 13 akiwa uhamishoni  huko Iraq, Imam Khomeini (MA) alilea na kuwafunza wanafunzi wengi na wakati huohuo kufichua maovu yaliyokuwa yakifanywa na utawala wa Shah kwa ushirikiano wa karibu na Marekani.

Baada ya kupamba moto mapambano na harakati za Kiislamu zilizokuwa zikiongozwa na Imam Khomeini dhidi ya utawala wa Shah, hatimaye Imam Khomeini alilazimika kutoka nchini Iraq na kuhamia Ufaransa, hadi Mapinduzi ya Kiislamu yalipopata ushindi nchini Iran hapo mwaka 1979.

Tangu yalipofikia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, taifa hili la Kiislamu limekumbwa na mashinikizo na njama za kila namna za madola ya kibeberu ya Magharibi na hasa Marekani, vikiwemo vikwazo mbalimbali  vya kidhuluma, vita vilivyoanzishwa na utawala wa Saddam Hussein wa Iraq na kuilazimisha Iran kupigana vita hivyo vya kulazimishwa kwa muda wa miaka minane katika mazingira magumu sana ya kususiwa ya kambi zote mbili za mashariki na magharibi duniani.  

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema katika moja ya hotuba zake kuwa,  ubunifu mkubwa zaidi wa Imam Khomeini ulikuwa ni kuunda na kuiasisi Jamhuri ya Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa,  kazi kubwa aliyoifanya Imam Khomeini ilikuwa ni kubuni fikra na nadharia ya Jamhuri ya Kiislamu na kuingiza nadharia hiyo katika uga wa siasa na kisha hatimaye kutekeleza nadharia hiyo kivitendo.

Ameongeza kuwa, katika mifumo mbali mbali ambayo imeundwa duniani katika kipindi cha takribani karne mbili zilizopita, hakujashuhudiwa mfumo ambao umetabiriwa kusambaratika kama ilivyotabiriwa kuhusu Jamhuri ya Kiislamu. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wale waliochukizwa na mapinduzi hayo walikuwa wanatabiri kuwa yataanguka au kusambaratika baada ya miezi miwili, sita au mwaka mmoja. Ameongeza kuwa, kusimama kidete kwa Imam Khomeini, misimamo yake imara, ushindi mkubwa wa taifa katika vita na masuala mengineyo, yote hayo yalibatilisha utabiri na ndoto za alinacha za mabeberu. Amesema kuwa baada ya kuaga dunia hayati Imam Khomeini maadui walikariri matarajio yao hayohayo ya kusambaratika Jamhuri ya Kiislamu. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa mitazamo kama hiyo ilitokana na uzoefu wa mapinduzi katika maeneo mengine ambayo yalianza kwa nguvu lakini yakawa na mwisho mbaya.

Ayatullah Khamenei amesema siri ya kubakia na umashuhuri wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni maneno mawili, Jamhuri na Kiislamu yaani wananchi na Uislamu. Amefafanua zaidi kwa kusema maana ya Jamhuri ni wananchi na maana ya Uislamu hapa ni mfumo wa Kiislamu unaotegemea kura za wananchi. 

Harakati za Imam Khomeini hazikuishia ndani ya mipaka ya Iran tu, bali hata katika uga wa kimataifa, kwani aliweka msingi imara wa kuwakutanisha Masuni na Mashia wakati wa mazazi ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAWW), kwa kuanzisha Wiki ya Umoja (12 Rabiul Awwal hadi 17 Rabiul Awwal). Pia, alikuwa mstari wa mbele katika kuwatetea na kuwaunga mkono Wapalestina, na kutangaza kila Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhan, ni Siku ya Kimataifa ya Quds.

Tunatoa mkono wa pole kwa Waislamu wote duniani kwa mnasaba huu mchungu wa kukumbuka siku aliyoaga dunia Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran.

 

 

تانزانیا دارالسلام

تانزانیا دارالسلام

Picha

Andika maoni yako.

Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ni moja ya mashirika ya Iran ambayo yanafungamana na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu; na ilianzishwa mwaka 1995. [Ziada]

Ingiza maandiko yako Kisha bonyeza Enter

Mabadiliko ya ukubwa wa maandiko:

badilisha nafasi za maneno:

Badilisha urefu wa mistari:

Badilisha aina ya panya: