Chuo Kikuu cha Isfahan

Chuo Kikuu cha Isfahan

Chuo Kikuu cha Isfahan

Chuo Kikuu cha Isfahan, ndio chuo kikuu cha kwanza  kuwepo katika eneo la katikati na kusini mwa Iran, ni moja ya vyuo vikuu viwili vikubwa vya umma vilivyopo  Isfahan na chuo kikuu kikubwa zaidi katika eneo la katikati mwa  nchi, na moja  kati ya vyuo vikuu vitano bora hapa nchini. Chuo Kikuu  cha Isfahan  chenye eneo la karibu hekta 2,300 ni moja ya vyuo vikuu vikubwa zaidi  hapa nchini. Chuo Kikuu hiki kina taasisi 5 za utafiti na vitivo 15.

Vitivo vya Chuo Kikuu cha Isfahan

• Kitivo cha Fasihi na Sayansi ya Binadamu

• Kitivo cha Theolojia na Maarifa ya Ahl al Bayt

• Kitivo cha Sayansi ya Michezo

• Kitivo cha Lugha za Kigeni

• Kitivo  cha Kemia

  Kitengo cha Jiolojia

• Kitivo cha Sayansi ya Utawala na Uchumi

• Kitivo cha Malezi na Saikolojia

• Kitivo cha Sayansi ya Jiografia na Mipango

• Kitivo cha Uhandisi na Usafirishaji

• Kitivo cha Uhandisi

 • Kitivo cha  Uhandisi wa Kompyuta

• Kitivo cha Sayansi ya Biolojia na Teknolojia

• Kitivo cha  Hisabati na Takwimu

• Kitivo cha Fizikia

 

Vituo vyaUtafiti

• Kituo cha Utafiti cha Mifumo ya Kiakili

• Kituo cha Utafiti wa Saikolojia ya Kiteknolojia

• Kituo cha Utafiti wa Bidhaa za Asili

• Kituo cha Utafiti wa Teknolojia ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari

• Kituo cha Utafiti wa Uhandisi wa Kimchakato

• Kituo cha Utafiti cha Alaa

Kulingana na takwimu iliyotolewa hivi karibuni  na  Kituo cha Uorodheshaji wa Vyuo Vikuu  Ulimwenguni (CWUR) mwaka 2021- 2022, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Isfahan kimepanda daraja 48 ikilinganishwa na mwaka jana, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Isfahan kinashikilia nafasi ya 694 kati ya vyuo vikuu ulimwenguni,kinashika nafasi ya pili kati ya vyuo vya teknolojia hapa nchini  na kilishikilia nafasi ya tano kati ya vyuo vyote vikuu hapa nchini Iran.

JIna Chuo Kikuu cha Isfahan
Nchi Iran
694
Anwani+98-313-7932003-7
Tovutihttps://ui.ac.ir/EN

Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ni moja ya mashirika ya Iran ambayo yanafungamana na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu; na ilianzishwa mwaka 1995. [Ziada]

:

:

:

: