• Aug 25 2023 - 12:21
  • 300
  • Muda wa kusoma : 1 minute(s)

Rais wa Iran Ebrahim Raisi akutana na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Iran Ebrahim Raisi akutana na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kando ya mkutano wa 15 wa kundi la nchi zinazoibukia kiuchumi za BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 24, 2023.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi akutana na Rais  wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kando ya mkutano wa 15 wa kundi la nchi zinazoibukia kiuchumi za BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 24, 2023.

Ikumbukwe Iran na Tanzania kwa muda mrefu imekuwa na ushirikiano katika maeneo mbalimbali, hadi sasa Iran na Tanzania inashirikiana katika sekta za elimu, afya, utalii, nishati, madini. Pia kwa sasa Iran imeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo hasa ukizingatia kilimo ni kipaumbele cha Serikali,”

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena  Tax aliwahi kusema kuwa, Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Iran katika maeneo mapya ya kimkakati ikiwemo sekta ya kilimo ili kupata uzoefu katika maendeleo na uwekezaji wa kuifanya nchi kuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha pamoja na kuongeza viwanda. 

 

Kuhusu biashara na uwekezaji, Dkt. Tax alisema kuwa kupitia kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji lililofanyika Mwezi Agosti, 2022 limefungua fursa za biashara na uwekezaji. “Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwavutia wafanyabiashara na wawekezaji wengi zaidi kuwekeza nchini,” alisema Dkt. Tax

تانزانیا دارالسلام

تانزانیا دارالسلام

Andika maoni yako.

Ingiza maandiko yako Kisha bonyeza Enter

Mabadiliko ya ukubwa wa maandiko:

badilisha nafasi za maneno:

Badilisha urefu wa mistari:

Badilisha aina ya panya: