MWANAZUONI MAARUFU WA HISTORIA YA KISHIRAZI
MWANAZUONI MAARUFU WA HISTORIA YA KISHIRAZI ATEMBELEA KUTOA CHA UTAMADUNI CHA IRAN
Prof. Abdul Shariff na ziara yake ndani ya kituo cha utamaduni cha Iran , ziara iliyolenga kuimarisha Historia muhimu ya Uajemi baina ya Iran na Tanzania

Tarehe 28 Julai 2025, Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania kilimpokea kwa mikono miwili Profesa Abdul Sheriff mwanazuoni mashuhuri wa historia ya Washirazi na mtafiti mahiri wa urithi wa kitamaduni wa Pwani ya Afrika Mashariki. Ziara yake ililenga kutembelea maonyesho maalum ya kituo hicho kuhusu urithi wa Washirazi, kushirikiana uzoefu wake mpana wa kitaaluma, pamoja na kuweka misingi ya ushirikiano wa baadaye katika kuendeleza na kuandika historia hii ya pamoja kati ya mataifa mawili; Iran na Tanzania.
Andika maoni yako.