• Jun 7 2022 - 01:45
  • 446
  • Muda wa kusoma : 4 minute(s)
Imam Khomeini RA

Kongamano la kumbukizi ya kifo cha Imam Khomeini (RA) lafanyika nchini Tanzania

Kwa mnasaba wa kukumbuka miaka 33 ya kufariki dunia Ayatullah Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kushirikiana na Idara ya Falsafa na Mafunzo ya Dini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Falah

Kwa mnasaba wa kukumbuka miaka 33 ya kufariki  dunia Ayatullah Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kushirikiana na Idara ya Falsafa na Mafunzo ya Dini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Falah ya Maendeleo ya Kiislamu  wamefanya mkutano  kwa ajili ya kumuenzi mtu huyo mkubwa na kufahamisha jamii fikra na falsafa yake ya Kiislamu. Mkutano huo ulikuwa fursa nzuri ya kumkumbuka shakhsia huyu mkubwa na kumtambulisha kwa kizazi kipya.

 

 

Bwana Morteza Pirani

Mzungumzaji wa kwanza alikuwa Bwana Morteza Pirani, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran, ambaye kwanza aliwakaribisha wageni na kusema kuwa:

Moja ya nadharia za Imam Khomeini (MA) ilikuwa ni kutoogopa madola makubwa, kwa sababu aliamini kwamba mamlaka kuu ya dunia iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na hatima ya wanadamu inaamuliwa na Mwenyezi Mungu.

Fikra nyingine  muhimu ya Imam Khomeini ilikuwa ni kusaidia mataifa yaliyokandamizwa. Kwa mfano, baada ya mapinduzi, Iran ilikabidhi ubalozi wa Israel mjini Tehran kwa serikali ya Palestina. Bw. Pirani aliongeza kuwa mfano mwingine wa Iran ni kukata uhusiano na Afrika Kusini wakati wa ubaguzi wa rangi  na kumuunga mkono Nelson Mandela hadi utawala  huo wa ubaguzi wa rangi ulipoondolewa madarakani.

 

Balozi wa Iran Hossein Alvandi

Naye Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Mheshimiwa Hossein Alvandi ametoa hotuba na kusema: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalitokana  zaidi ya karne moja ya mapambano ya wananchi Waislamu dhidi ya ukoloni na ukndamizaji nchini humo. "  Ameongeza kuwa, bila ya shaka, bila ya kuwepo uongozi wenye mvuto na usioweza kuyumbishwa wa Imam Khomeini, mapinduzi haya yasingefanikiwa kamwe, na kwa mujibu wa  maelezo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhma  Khamenei, mapinduzi haya yasingeweza kujulikana popote duniani bila ya jina la Imam Khomeini.

Moja ya malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ilikuwa ni kuleta umoja na mshikamano wa nchi zinazoendelea na zile zinazokandamizwa. Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kuanzisha uhusiano barani Afrika baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Kuanzisha na kuendeleza uhusiano na Tanzania na kusaidia ustawi  na maendeleo ya nchi hii,  yalikuwa ni matokeo ya awali ya Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na Imam Khomeini.

Dk. Josephat Muhoza

Dk. Josephat Muhoza, Mhadhiri wa Falsafa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema Imam Khomeini alikuwa kiongozi na aliweza kutekeleza majukumu yake ya uongozi tangu mwanzo wa mapambano dhidi ya utawala wa Shah hadi alipopelekwa uhamishoni. Hatimaye Imam Khomeini alirejea Iran, akachukua uongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kuupindua utawala wa kifalme.

Dakta Seyyed Mehdi Khamoushi

Pia Dakta Seyyed Mehdi Khamoushi Mkuu wa Taasisi ya Wakfu  ya Iran amesema miongozo na mienendo ya kisiasa ya Imam Khomeini (MA) ni tafsiri ya wazi ya falsafa ya kisiasa ya Uislamu. Dakta Khamoushi amesema kuwa, nadharia ya Uislamu wa kisiasa ni nadharia ambayo imewasilishwa kutoka katika mkusanyo wa kauli na miongozo ya Imam Khomeini kuwa ni mwana itikadi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ili kuutoa ulimwengu wa Kiislamu katika kubaki nyuma na kuuelekeza kwenye  maendeleo kwa maslahi ya hapa  duniani  na akhera. Dakta Khamoushi amesema, nadharia ya Uislamu wa kisiasa imepata nafasi ya juu katika akili za wasomi na imefungua upeo mkubwa  wa matumaini katika mtazamo wao.

 

Sheikh Mulabah Swaleh

Sheikh Malabah Swaleh, mmoja kati ya  wanazuoni wa Kishia nchini Tanzania amesema: “Imam Khomeini alikuwa mwalimu mzuri wa maadili na tabia yake ilikuwa ni mfano mzuri kwa wanafunzi wake, watu wa Iran na watu wote  duniani. Wakati nchi za Magharibi zinautuhumu Uislamu kwa kukiuka haki za binadamu na kanuni za maadili, kuna sheria za ajabu zimewekwa katika nchi za Magharibi zinazoruhusu ndoa za jinsia moja, jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya dini zote za mbinguni. Ameongeza kuwa, serikali za kibeberu zinawalazimisha viongozi wa nchi zinazoendelea hususan nchi za Kiafrika kufanya wanayoyataka, ikiwemo  kupora mali na mengineyo na viongozi hao hawana sauti ya kupinga wala kukataa, lakini Imam Khomeini alikuwa hakubali kufuata kibubusa matakwa ya Wamagharibi.

 

Bwana Qassim Hassan Ntabindi

Naye Bwana Qassim Hassan Ntabindi  alilaani njama za vyombo vya habari vya Magharibi vya kuchafua sura ya Uislamu duniani na kusema kuwa, iwapo Waislamu watashikamana na mafundisho ya dini hiyo tukufu, madola ya kibeberu  duniani  hayataweza kuwadhuru. Ameongeza kuwa, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini hakuifanya Iran kuwa nchi ya Wairani tu, bali aliifanya kuwa kimbilio la mataifa yote ya duniani. Kwa ajili hiyo, miezi sita tu, baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni Siku ya Quds Duniani, yenye lengo la kuukomboa Msikiti huo Mtakatifu kutoka katika makucha ya Wazayuni wa Israel.

 

Dr. Avazeli Lwaitama

alizungumzia zaidi utu na kukuhusu Imam Khomeini pia alikuwa na utu ndio mana watu wa Iran walikuwa wana kubali na kumuheshimu sana, ndio aliposema mimi nina wa na akawabidhi wananchi wa Iran kuunda serikali wanayoitaka, akasema hakika Imam Khomeini alikuwa ni mchamungu wa kweli na hakuna na tamaa ya madaraka kama ambavyo ilivyokuwa kwa Shaha alikuwa na uchu wa madaraka na kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi.Lakini Imam Khomeini alikuwa ni mtu muadilifu sana na hakupenda dhulma sio kwa waislamu tu bali kwa binadamu wote na ndio maana alikuwa anasaidia taifa la Palestifa kutokana na madhili ya wazayuni walowezi wa ardhi za wapalestina

 

Dr. Ahmad Khatibu

Yeye alizungumzia zaidi Imam Khomeini haswa walipokuwa Ufaransa namna Imam Khomeini alivyokuwa mnyenyekevu hata chai alikuwa akiwasevia wageni wake kwa mkono wake mwenyewe, 

 

تانزانیا دارالسلام

تانزانیا دارالسلام

Andika maoni yako.

Ingiza maandiko yako Kisha bonyeza Enter

Mabadiliko ya ukubwa wa maandiko:

badilisha nafasi za maneno:

Badilisha urefu wa mistari:

Badilisha aina ya panya: