Bunge la Iran lawasili Tanzania
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Kilimo, Maji, Maliasili na Mazingira kutoka Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 5 Septamba, 2023.

ikumbukwe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian aliwahi kufanya ziara nchini Tanzania na kuonana na viongozi wa ngazi za juu wa Tanzania, akiwemo Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dokta Hussein Ali Hassan Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitembelea Tanzania ikiwemo Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake katika nchi ya magharibi mwa Afrika ya Mali na hiyo ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.
Wakati wa mazungumzo yake na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Amir-Abdollahian aliashiria uwezo mkubwa wa Iran kiuchumi hasa katika nyuga za biashara, nishati, viwanda, teknolojia na vyuo vikuu na ametoa mwito wa kuondolewa vikwazo kwa mashirika na wafanyabiashara wa Iran nchini Tanzania hasa katika masuala ya visa.
Andika maoni yako.