Muhammad bin Hassan Jahrudi

Muhammad bin Hassan Jahrudi

Muhammad bin Hassan Jahrudi
Muhammad bin Hassan Jahrudi anayejulikana kwa jina la Khajeh Nasir Din Tousi, (Tusi) msomi na mwanatheolojia wa Kiislamu, alizaliwa katika mji wa Tous mnamo tarehe 11 Jamadi al-Awwal mnamo 597 Hijria nchini Iran, na jina la "Tousi" linamaanisha mahali alipozaliwa.
Khajeh Nasir Din Tousi ni malenga na mshairi maarufu wa Kiirani wa karne ya saba, ambaye pia amebobea kwenye fani mbalimbali na kuhesabiwa kuwa ni mwanafalsafa, mwanatheolojia, mwanasheria, mnajimu, mwanafikra, mwanahisabati, daktari na mbunifu.
Khajeh Nasir Din Tousi ni mmoja wa wanasayansi ambaye, pamoja na ustadi wake wote katika Sayansi, pia alikuwa Malenga na Mwandishi wa Mashairi. Mashairi yake mengi yalikuwa yamejikita zaidi katika mada za kifalsafa, kiirfani, kinajimu na kimaadili.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, kila mwaka ifikapo Tarehe 5 ya mwezi wa Esfand (Kalenda ya Kiirani), sawa na tarehe 24 Februari, hufanyika kumbukizi ya Mwanasayansi huyu Mashuhuri Khajeh Nasir Din Tousi, kama Siku ya Mhandisi.
JIna Muhammad bin Hassan Jahrudi
Nchi Iran
Jina la Utani Khajeh Nasir Din Tousi
Wakati wa UzalishajiKarne ya Saba
kaziMuhammad bin Hassan Jahrudi anayejulikana kwa jina la Khajeh Nasir Din Tousi, (Tusi) msomi na mwanatheolojia wa Kiislamu, alizaliwa katika mji wa Tous mnamo tarehe 11 Jamadi al-Awwal mnamo 597

Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ni moja ya mashirika ya Iran ambayo yanafungamana na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu; na ilianzishwa mwaka 1995. [Ziada]

Ingiza maandiko yako Kisha bonyeza Enter

Mabadiliko ya ukubwa wa maandiko:

badilisha nafasi za maneno:

Badilisha urefu wa mistari:

Badilisha aina ya panya: