Wiki ya Umoja wa Kiislamu

Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema hilo la kila mwaka Iran inafanya kongamano la
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema hilo la kila mwaka Iran inafanya kongamano la umoja wa Kiislamu ambapo nchi zaidi ya 50 hualikwa katika kongamano hilo. Hualikwa Mamufti na wanazuoni pamoja na wasomi wa ngazi za juu wa ulimwengu wa Kiislamu.
Halikadhalika kuna idadi kubwa ya wanazuoni na wanaharakati wanaoshiriki katika kongamano hilo kwa njia ya intaneti.
kauli [M1] mbiu ya kongamano la mwaka huu ni, “Umoja wa Kiislamu, Amani na Kuzuia Mifarakano na Mizozo katika Ulimwengu wa Kiislamu.”
kwa kuzingatia masaibu ya ulimwengu wa Kiislamu kama vile vita, umwagaji damu na ugaidi kwa kawaida hujadiliwa mada muhimu kama ya ‘Vita na Amani Yenye Uadilifu’. Mada zingine zinazopewa umuhimu ni pamoja na Palestina na Mapambano ya Kiislamu, Udugu wa Kiislamu, Kukabiliana na Ugaidi, Kuheshimiana Wafuasi wa Madehebu za Kiislamu, Umma Moja, na Muungano wa Nchi za Kiislamu.